Ulinzi Dhidi ya Kukata tamaa

Teaching Legacy Letter
*First Published: 2011
*Last Updated: Februari 2026
12 min read
Mara ya kwanza nilipomsikia Billy Graham akizungumza alikuwa London mnamo mwaka wa 1954. Jambo moja alisema kwenye ibada hiyo sikuwahi kusahau. Alisema, “Mungu kamwe hamtumii Mkristo aliyekata tamaa.” Nilifikiria juu ya jambo hili na kuhitimisha kwamba hiyo haikuwa sawa kabisa. Mimi mwenyewe nilikuwa nakabiliwa na tatizo la kukata tamaa siku hizo, na nilifikiria haikuwa vizuri sana kwake kusema hivyo.
Mfano alioutoa ni Gideoni akiwa ameketi kwenye shinikizo la mvinyo, akipepeta ngano na kujificha kwa kukata tamaa kabisa. Malaika wa Bwana alimtokea Gideoni na taarifa isiyotarajiwa, akamwambia, “Bwana yu pamoja nawe, Ewe shujaa mwenye nguvu.” Waamuzi 6:12. Kwa kweli, Gideoni alitazama pande zote kuona ni nani malaika alikuwa akizungumza naye, kwa sababu alikuwa akitetemeka kwa hofu ya Wamidiani. Ilimbidi Bwana abadilishe maoni yake Gideoni kijihusu mwenyewe kabla ya kufanya chochote naye.
Vivyo hivyo ni kweli kwetu. Ikiwa hatuwezi kujiangalia kupitia macho ya imani, basi hatufai kwa huduma ya Mungu. Maoni yetu yasio sahihi kutuhusu yatafadhaisha kila kitu ambacho Mungu anataka kutufanyia tusipoangalia mambo kwa mtazamo tofauti. Kimsingi nataka kuzungumza nawe juu ya jibu la kukata tamaa kulingana na Maandiko na jinsi ya kukabiliana na aina hiyo ya shambulizi la kiroho.
Vifaa Tunavyohitaji
Sura ya sita ya Waefeso imeorodhesha vifaa sita vya kijeshi: mshipi wa kweli, dirii ya haki, viatu vya injili ya amani, ngao ya imani, chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho. Haya sio tu majina ya dhana au hila za kitheolojia. Ni hali halisi za vitendo ambazo kila mmoja wetu anahitaji kushikilia. Ningependa kuchukua vifaa viwili kati ya hivyo sita na kukupa mafundisho fulani ya vitendo kutoka kwa Maandiko kuhusu ya jinsi ya kupinga uvamizi wa kukata tamaa kiroho.
Kwa maana kushindana kwetu sio dhidi ya mwili, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara. Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, nayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani. Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu. (Waefeso 6: 12-17)
Kwa msingi wa masomo yangu na tafsiri nyingi za kisasa, ninaamini kwamba aya ya kwanza inaweza kusomwa kwa usahihi zaidi: "Kwa maana mechi yetu ya mieleka sio dhidi ya watu walio na miili." Hilo ni dhahiri sana. Kwa maneno mengine, hatupigani dhidi ya wanadamu. Mama mkwe wako sio tatizo, au hata dikteta kama Stalin au Hitler.
Kupigana kwetu sio dhidi ya watu wenye miili, lakini dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Vaeni Silaha Zenu
Tunashiriki katika mapambano na watu wa kiroho wasioonekana ambao wana nguvu kubwa, walio na utaratibu wa hali ya juu na wanapingana nasi kabisa kwa kila kitu kinachosimamia Mungu na watu wa Mungu. Makao yao makuu yapo mbinguni, na wanatoa kila aina ya shinikizo la kiroho dhidi yetu ambalo kwa njia yoyote litatushusha chini. Kama hitimisho la ukweli huo, Paulo anasema katika aya ya 13, Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara. Huo ni uhitimisho wa kimantiki na wa vitendo.
Nisingependekeza mtu yeyote ajihusishe katika vita vya kiroho au katika kujenga Ufalme wa Mungu bila kwanza kuvaa silaha. Kwa nini? Kwa sababu wakati unaposhambulia ibilisi, Kumbuka kwamba imani ya maandiko huwa daima niamini, atalipiza kisasi na hafuati sheria.
Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja.( Waefeso 6:13 )
Tazama kwamba Paulo anafikiria siku ya uovu inakuja. Siamini kuwa hii inahusu Dhiki kuu. Inamaanisha kwamba kila Mkristo atapitia siku yake ya uovu. Wakati Yesu alitoa mfano wa watu wawili ambao walijenga nyumba, mmoja juu ya mwamba na mwingine juu ya mchanga (Mathayo 8: 24-27), Hakusema, “Ikiwa upepo na mvua zinakuja.” Alisema, “Wakati upepo na mvua zitakapokuja.” Kila nyumba ilikumbana na mazingira sawa.
Wakati Yesu alitoa mfano wa mpanzi, alisema, “dhiki au mateso yanapoinuka” Mathayo 13:21. Hakusema “ikiwa.” Alichukulia kawaida kwamba mateso yatakuja. Kila Mkristo atalazimika kupitia siku ya uovu wakati atakabiliwa na dhiki na kuteswa. Kama Paulo alivyosema katika Matendo 14:22, “Lazima kupitia dhiki nyingi tuingie katika ufalme wa Mungu.” Hakuna njia nyingine.
Kwa hivyo, kwanza kabisa, tunahitaji kuelewa wakati na kuweka katika akili zetu. Kumbuka kuwa haimaanishi Kuna kitu kibaya wakati tunajikuta katika siku ya uovu, na shinikizo kubwa. Haimaanishi kuwa sisi tuko nje ya mapenzi ya Mungu. Badala yake, labda ni ishara nzuri kwamba tuko njiani kuingia kwenye Ufalme wa Mungu.
Kati ya vifaa sita vinavyoorodheshwa na Paulo, mimi nataka tu kuzungumza juu ya viwili: dirii na ngao. vingine vinne ni muhimu, lakini kwa madhumuni ya barua hii, nataka kuzingatia vile viwili ambavyo nimetaja. Ninataka kuchunguza kwa njia ya vitendo sana - haswa kutokana na uzoefu wa kibinafsi- matumizi ya dirii na ngao.
Dirii
Kuanza, hebu tuangalie kifungu kinachofanana cha sehemu ya Waefeso 6 katika 1 Wathesalonike 5:
Lakini kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukijivika imani na upendo kama dirii kifuani na tumaini letu la wokovu kama chapeo. (1 Wathesalonike 5: 8)
Waefeso 6:14 inasema, dirii ya haki kifuani lakini 1 Wathesalonike 5: 8 inatuambia zaidi haki hiyo ni nini. Sio haki ya kujitahidi au matendo mema lakini ni haki ya imani ambayo inafanya kazi kwa upendo. (Mada hii ya imani, ni muhimu kwa silaha hizi na pia kwa viungo muhimu vya mwili ambavyo hulindwa.)
Ni kiungo gani muhimu cha mwili ambacho dirii inalinda? Moyo. Kinga ya moyo ni kusudi la dirii ya haki kupitia imani ambayo inafanya kazi kwa upendo. moyoni, sio kichwani. Kwa mfano, Warumi 10:10 inasema, Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, Imani ya kweli sio tu dhana za kielimu wala theolojia au fundisho. Ni imani ya moyo ambayo inafanya kazi katika mstari mmoja wa msingi - upendo.
Kwa kushirikiana na hii, angalia Wagalatia 5: 6:
Kwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.
Hiyo ni taarifa rahisi, lakini yenye uzito. Tunahitaji kujikumbusha kila wakati kuwa kitu pekee ambacho ni cha muhimu sana katika maisha yote ya Kikristo ni imani ambayo inafanya kazi kwa upendo. Tunaweza kuwa na majibu kwa maswali ya kitheolojia na bado tunakosa ukweli huu mkuu imani katika moyo unaofanya kazi kwa upendo. Bila hiyo, umekosa yote.
Dirii inayolinda moyo ni imani ambayo inafanya kazi kupitia upendo. Mara tu dirii hio inapoondolewa, Kiungo chetu muhimu zaidi, moyo, hubaki wazi.
Kuhusu asili ya imani, tunahitaji kuona kwamba daima inahusiana na visivyoonekana na sio na vinavyoonekana. Kama 2 Wakorintho 5: 7 inasema, kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona. Kuenenda kunamaanisha “kuishi.” Maisha yetu yote kama Wakristo hayatokani na yale tunayoona, lakini kwa kile tunachoamini. Ni kwa imani, sio kwa kuona, na hizi mbili zinapingana. Ikiwa tunaishi kwa yale tunaona, hatuishi kwa kile tunaamini.
Swala zima lilikuwa kosa la kwanza kabisa ambalo binadamu alifanya. Wakati nyoka katika Bustani ya Edeni alihoji neno la Mungu, na kisha Eva kukubali swali hilo, alishindwa. Mwanzo 3: 6 inatuambia ni shinikizo gani Eva alijibu: Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula. Neno kuu hapo ni alipoona. Eva aliondoka kutoka katika ulimwengu wa imani katika neno lisiloonekana hadi kuamini kuona kwake; Mara baada ya hilo, alishindwa. Kanuni hio hio inatumika kwetu. Tunapoenda kwa kile tunachoona, shetani anatushinda. Lazima tutembee kwa imani, sio kwa kuona.
Dirii ambayo inalinda mioyo yetu ni imani kwa Mungu asiyeonekana na neno Lake, na imani hii inafanya kazi kwa upendo. Wakati tunaachana na imani hiyo, tunaacha kuwa na upendo wa kweli. Watu wengine wanasema, “Upendo ni muhimu zaidi kuliko imani.” Hiyo inaweza kuwa kweli, lakini njia pekee ya kupenda ni kwa imani. Kwa kuwa imani inafanya kazi kwa njia ya upendo, haishangazi tunakasirika, kufadhaika, kukosa uvumilivu, na kuwafokea wenzi wetu wakati tu tunaachilia dirii. Imani yetu, ambayo ndiyo kitu pekee ambacho hutoa upendo, inaondoka. Kwa sababu hiyo, hutokea yule mtu wa zamani na tabia zake zote za zisizopendeza. Lakini shida ya msingi ni nini? Dirii imewekwa chini.
Ngao
Ikiwa dirii inalinda moyo, ngao inalinda mwili mzima. Katika enzi ya Warumi, ikiwa ulijua jinsi ya kutumia ngao, hakuna sehemu yako ingeweza kufikiwa na mishale ya moto. Vivyo hivyo ngao ya imani inalinda mwili mzima.
Wakati mwingine hatuelewi imani, tukifikiria kama kitu tunapaswa kufanya kwa uangalifu wakati wote. “Lazima ninyooshe misuli yangu ya kiroho na kuamini.” Lakini imani sio kitendo bali ni tabia ya kumtegemea Mungu.
Mke wangu marehemu Lydia alikuwa akitoa mfano wa mvulana mdogo mikononi mwa baba yake. Mvulana yule angeshikilia sana koti la baba yake ili asianguke, lakini baada ya muda alisinzia na kuacha koti. Mikono yake ingepumzika, lakini baba yake bado alikuwa akimshika. Juhudi za mvulana huyu za kushikilia koti kweli hazikuwa muhimu. Hivyo ni kama sisi na Mungu. Tunaweza kushikilia, lakini hata tunapoachilia, Mungu bado anashikilia.
Kwa njia fulani, tunaweza kupumzika. Imani sio juhudi ya kuendelea kushikilia Mungu asije akaondoka. Badala yake, ni mtazamo wa kujua kwamba Mungu yuko, na chini kuna mikono Yake ya milele. Pamoja na mtazamo huo, kuna uthibitisho wa imani uliyonayo.
Labda umesikia juu ya mafundisho haya ya kawaida sana.Ambayo ni: Ukweli, Imani na Hisia, kwa utaratibu huo. Ukweli uko katika Biblia, imani inathibitisha ukweli huo, na hisia zako zinajishughulikia. Lakini ikiwa tutaanza na hisia zetu, tutakuwa wasio na msimamo kama hisia hizo. Ukweli haubadiliki hisia hubadilika mara kwa mara.
Hatuwezi kumudu msingi wa imani yetu kwa hisia zetu. Weka msingi wa imani yako kwa ukweli katika Neno la Mungu, ambalo halibadiliki wakati wote. Kuamini hilo inahitaji uamuzi wa kiakili. Smith Wigglesworth aliwahi kusema, “Sivutiwi na kile ninahisi; ni kwa kile tu ninaamini.”
Chanzo cha kweli, kisichobadilika na halali ni ukweli wa Biblia. Imani inasema, “Biblia ni kweli na ninaiamini. Mungu yuko hapa. Yeye hataniacha. Hisia zangu zinaweza kujishughulikia. “ Ikiwa una mtazamo huo, hisia zako zitaambatana na ukweli. Lakini ukianza na hisia zako, hautawahi kupata ukweli. Ni muhimu kabisa kuanza na ukweli katika Neno la Mungu.
Kufahamu Ukweli
Ili kufanya hivyo, lazima ujue ukweli. Lazima uwe na ufahamu wa yale maandiko yanasema.
Kwa mfano, ukweli wa ukombozi wetu. Neno ukombozi linamaanisha “kununua tena.” Maandiko yanasema kwamba tuliuzwa chini ya dhambi katika soko la watumwa la Shetani, lakini Yesu alitukomboa, au alitununua tena, katika soko la watumwa la Shetani na damu yake ya thamani. Ni wapi inasema ukweli huo? Zaburi 107 Aya ya 2 inasema, Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi, wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui, Bwana ametukomboa ili tusiwe mikononi mwa adui bali mikononi mwa Bwana.
Kisha tazama Wakolosai 1: 12-14:
Mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru. Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa, ambaye katika yeye tunao ukombozi, yaani msamaha wa dhambi.
Ni ukweli kwamba Mungu ametukomboa kutoka kwa nguvu za giza- ufalme wa Shetani - na kutuweka kwa Ufalme wa Kristo. Kwa hivyo, tuna ukombozi na dhambi zetu zimesamehewa. Hatuko tena katika himaya ya Shetani wala hatuko chini ya mamlaka Yake. Wasioamini, wakataa Kristo, waasi na wasiotii wako chini ya mamlaka halali ya Shetani. Lakini sisi hatupo chini ya mamlaka ya shetani.
Ukweli ni kwamba wakati tulitubu na kujisalimisha kwa Yesu Kristo na kumfanya Bwana, tulibadilishwa, roho na mwili kutoka kwa ufalme wa Shetani na kuingia kwenye Ufalme wa Kristo.
Huu ni ukweli. Tunaamini ukweli kutoka kwa ulimwengu usioonekana wa Neno lake kwa sababu hatuendi tena kwa hisia zetu. Ngao hiyo ya imani inashughulikia kila eneo la maisha yetu. Hakuna mshale wa moto unapita.
Tunaweza kuona, basi, kwamba Mungu ametupatia kinga nzuri wakati adui anajaribu kutukatisha tamaa. Tunapokumbuka kujitayarisha kila siku kwa kuvaa silaha kama kinga dhidi ya shambulizi ambalo hakika litakuja (na mengine manne pia), tutapata Mungu akiwa mwaminifu ili kuimarisha imani yetu na tumaini, akituwezesha kusimama kwa ushindi katika Roho wake.
Koda: TL-L083-100-SWA