Tukikabiliwa na ufunuo wa Maandiko Matakatifu kuhusu uasiwa Shetani na malaika zake dhidi ya Mungu, tunawezakujiuliza kwa mshangao: “Je, Mungu hangeweza tu kuuzimauasi huo papo hapo na kumtupa Shetani pamoja na malaikazake wote katika ziwa la moto wanapostahili?”

Bila shaka, Mungu angeweza kufanya hivyo, lakinihakuchagua kufanya hivyo. Katika hekima yake isiyo nakifani, Mungu alimruhusu Shetani, hata katika uasi wake,kuwa chombo ambacho Angekitumia kutimiza makusudiYake. C.T. Studd, mchezaji wa kriketi Mwingereza aligeukakuwa mmisionari, alisema hivi: “Mungu amemtumia Shetanizaidi kuliko kiumbe kingine chochote alichokiumba.”

Ni kanuni katika jinsi Mungu anavyoshughulika nasi: uhusianowetu Naye hauwezi kuwa thabiti hadi tupitie majaribu fulaniambayo Yeye mwenyewe ameyaruhusu. Kanuni hii inawahusumalaika na wanadamu. Uhusiano ambao haujajaribiwa ni kama dhahabu ambayo haijasafishwa,haikubaliki mbinguni.

Ndiyo maana Yesu aliwaambia Wakristo wa Laodikia:“Nakushauri ununue kutoka kwangu dhahabu iliyosafishwakwa moto.”1 Kwa maneno mengine, Yesu alikuwa akisema,“Madai yenu ya kuwa watu Wangu hayana uzito mpakamtakapopitia jaribu na kusafishwa.”

Dhahabu ya aina hiyo siya bure na tunapaswa kuinunua kwa gharama, kwa maanakuna bei ya kulipa katika safari ya uaminifu na utiifu kwaMungu!

Shetani Mjaribu

Chombo kimoja kikuu ambacho Mungu hutumia kutujaribu niShetani. Mara mbili katika Maandiko anaitwa “mjaribu.”2 Hililinaweza kutafsiriwa kihalisi mjaribu.

Katika tukio la kwanza Mungu alimtumia Shetani kamamjaribu wake kati ya malaika mbinguni. Ni wale tu malaikawaliokataa kujiunga na Shetani katika uasi wake ndiowalioshinda jaribu hilo. Mara tatu Maandikoyanapozungumzia kurudi kwa Kristo katika utukufu nahukumu atakazozitoa, yanataja kwamba ataandamana namalaika watakatifu.3 Malaika hawa watakatifuwanatofautishwa na wale waliomuunga mkono Shetani katikauasi wake na kwa hiyo wakapoteza utakatifu wao.

Mungu pia hutumia Shetani kuwajaribu wanadamu. Hilililianza tangu mwanzo na Adamu na Hawa. Mungu aliwawekakatika bustani na kuwapa amri moja tu ya kuepuka: wasilematunda ya mti wa maarifa ya mema na mabaya. NdipoShetani akaingia katika bustani na kuwajaribu kufanya jambolile pekee ambalo Mungu alikuwa amelikataza. Walipoangukiajaribu hili, Mungu alitangaza hukumu kwa wote watatu.Shetani alikuwa ametekeleza jukumu lake alilopewa kamamjaribu, lakini Adamu na Hawa walikuwa wameshindwakatika jaribu lao. Kwa hili wao pekee waliwajibika.

Hata katika maisha ya Yesu Mwenyewe, Shetani aliruhusiwakuchukua nafasi ya mjaribu.

Baada ya Yesu kufunga siku arobaini nyikani, mjaribu alikujakwake na kumtia katika majaribu mara tatu mfululizo.4 Lakinipale ambapo Adamu wa kwanza alishindwa, Adamu wamwisho (Yesu Kristo) alishinda. Alipita majaribu yote matatukwa ushindi na ilimbidi Shetani arudi nyuma.

Miaka mitatu na nusu baadaye, Shetani aliendelea tena najaribu lake dhidi ya Yesu. Kwanza, aliingia ndani ya YudaIskariote na kumtumia kumsaliti Yesu” Kisha akachocheakundi la watu waovu kudai Yesu asulubiwe.

Ni hapo ndipo hekima kuu ya Mungu isiyoelezeka ilionekanakwa utimilifu wake.Kifo cha upatanisho cha Yesu msalabani kilifuta madai yoteya Shetani dhidi ya wanadamu walioanguka.Kile kilichoonekana kama ushindi wa Shetani kikawa ndiyochanzo cha kushindwa kwake kabisa..

Kutoka kwa Watumwa hadi Washindi

Lakini Mungu alikuwa bado na mpango mwingine wakuonyesha hekima Yake kuu.Shetani alikuwa amemshawishi mwanadamu kuasi, na kwanjia hiyo akawafanya watumwa wake.Lakini kupitia dhabihu ya upatanisho ya Yesu msalabani,Mungu hakutuokoa tu kutoka dhambini na kutufanya warithiwa Ufalme Wake, bali ametugeuza kuwa vyombovinavyotumika kumshinda Shetani. Watumwa wa Shetaniwanageuzwa kuwa washindi wake.Hakika, ni Mungu pekeeangeweza kupanga jambo la ajabu kama hilo!

Katika Katika Ufunuo 12:7–11, Yohana anaelezea vita vyambinguni—vita vya siku zijazo—ambavyo vitamaliza kabisaufalme wa Shetani na malaika wake waasi:

“Basi palikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika

wake wakapigana na hilo joka, nalo joka pamoja namalaika wake likapigana nao. Lakini joka na malaikawake wakashindwa, na hapakuwa tena na nafasi yaohuko mbinguni. Lile joka kuu likatupwa chini, yulenyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani,aupotoshaye ulimwengu wote. Akatupwa chini duniani,yeye pamoja na malaika wake. Kisha nikasikia sauti kuumbinguni, ikisema: “Sasa wokovu na uweza na ufalmewa Mungu wetu umekuja, na mamlaka ya Kristo wake.Kwa kuwa ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu,anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana. Naowakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwaneno la ushuhuda wao. Wala wao hawakuyapenda

maisha yao sana, hata wakawa tayari kufa.’”

Ufunuo huu unaonyesha mambo muhimu sana::

  1. Kabla ya wakati huu, Shetani na malaika zake

walikuwa bado na ufalme wao katika ulimwengu waroho.

  1. Maneno “ndugu zetu” yanayosemwa mbinguni

yanarejelea waamini walio duniani.

  1. Shetani na malaika zake hawakutupwa nje mpaka

waliposhindwa na nguvu ya pamoja ya malaika waMungu mbinguni na waamini duniani.

Hii inaelekeza kwenye kilele cha kustaajabisha cha pambanohilo: “Nao wakamshinda [Shetani].” Ni waaminiwaliokombolewa duniani wanaohusika katika kumtoa Shetanikabisa katika nafasi yake ya kifahari mbinguni. Waathirika wa Shetani hatimaye wanamshinda yeye.

Vita vinapiganwa kwa silaha za kiroho. Silaha kuu ya Shetanini hatia. Ndio maana anatushitaki mbele za Mungu mchanana usiku. Anamkumbusha Mungu dhambi zote tulizofanya.Kusudi lake ni kuendelea kusisitiza hatia yetu. Ikiwa kwelituna hatia, basi hatuna uwezo dhidi yake na hatuna haki yakuchukua mahali pake mbinguni.

Ushindi wetu unakuja pale tunapotumia silaha mbili kuuambazo Mungu ametupa: damu ya Mwana-Kondoo na nenola ushuhuda wetu. Damu ya Mwana-Kondoo inathibitishadhabihu ya kutosha ambayo Yesu aliitoa msalabani kwa niabayetu. “Kwa toleo moja amewafanya wakamilifu hata milelewale wanaotakaswa.”6 Dhabihu ya Yesu kwa ajili yetuinatosha milele. Hakuna kinachoweza kuongezwa walakupunguzwa. Matamshi ya mwisho ya Yesu msalabaniyalikuwa “Imekwisha!”7 Yaani, kila kitu kimetimizwa kikamilifu.

Mfano wa Pasaka

Mpango wa Mungu wa kutuokoa katika pambano hili lanyakati za mwisho ulionyeshwa kinabii kupitia sherehe yaPasaka, ambapo Mungu aliwakomboa Waisraeli kutokautumwa wa Misri. Mwana-kondoo wa Pasaka alikuwa mfano wa Yesu Kristo,Mwana-Kondoo wa Mungu.”

Kila baba wa Kiyahudi alipaswa kuchagua mwana-kondooasiye na doa, kumchinja, na kukusanya damu yake kwenyechombo.Lakini kazi haikuishia hapo.Damu iliyokuwa ndani ya chombo haingeweza kumlindayeyote.Ilipaswa kupakwa kwenye kizingiti na miimo miwili ya mlangowa kila nyumba ya Mwisraeli.Mungu alikuwa ameahidi: “Nitakapoiona damu, nitapita juuyenu,”8 yaani, “Hivyo hukumu haingewagusa waliokuwandani ya nyumba iliyotiwa damu.”

Kipengele cha mwisho muhimu katika sherehe ya Pasakakilikuwa mmea uitwao hisopo, unaokua kwa wingi katikaMashariki ya Kati.Baba wa familia alipaswa kuchuma tawi la hisopo, kulichovyakwenye damu iliyo kwenye chombo, kisha kuipaka damu hiyokwenye kizingiti na miimo ya mlango.Ni baada ya hatua hiyo tu ndipo nyumba hiyo ilikuwa salama.

Vivyo hivyo, Yesu alipomwaga damu Yake msalabani kwa ajiliyetu, damu hiyo sasa iko kwenye “chombo.”Lakini damu iliyo kwenye chombo haiwezi kumlinda mtuyeyote.Inapaswa kutumika mahali tunapoishi — ndani ya maishayetu.

Katika sherehe ya Pasaka ilikuwa ni hisopo iliyopaka damupale ilipohitajika. Katika maisha yetu ya kiroho, ninikinachochukua nafasi ya hisopo?Jibu linapatikana katikaUfunuo 12:11:

Jibu linapatikana katikaUfunuo 12:11:Ushuhuda wetu binafsi ndio hisopo letu la kiroho. Tunaposhuhudia kwa imani kile ambacho damu ya Yesuinafanya kwa ajili yetu, ndipo tunapata ulinzi na baraka zoteambazo Mungu ametupatia kupitia dhabihu ya Kristo.

Ushuhuda wetu wa ujasiri na wa kudumu unakuwa hisopolinalopaka damu ya Yesu katika maisha yetu.Hata hivyo, lazima tukumbuke kwamba Shetani naye anajuaMaandiko.Anaujua mpango wa Mungu, na anatambua kwamba Munguanawatumia waamini duniani kama chombo cha kumshinda.Ndiyo maana mkakati wake ni kutufanya tuishi katika hatia,kujiona wasiostahili na wasiofaa.Kwa sababu hiyo, anatushitaki mbele za Mungu mchana nausiku.”9

Tunaweza kuuliza: Kwa nini Mungu hanyamazishi mashtakaya Shetani? Jibu ni kwamba Mungu hatufanyii kile ambachoametupa uwezo wa kufanya sisi wenyewe.Ametupatia silaha za kiroho ambazo zinaweza kushinda kilashtaka ambalo Shetani analeta dhidi yetu.Kwa kila shtaka la Shetani, tunaweza kujibu kwa imani: Damuya Yesu iliyomwagika msalabani imeniosha na kunisafishakabisa. Kwa hiyo, mimi si mwenye hatia!

== Mwongozo kwa Wanajeshi wa Wakati waMwisho ==

Kama ilivyo katika jeshi la duniani, askari anayeandikishwahupewa silaha zake na kisha hufundishwa kuzitumia kwaustadi.Vivyo hivyo, kama askari katika jeshi la Bwana katika siku hiziza mwisho, ni lazima tujifunze kutumia kwa ufanisi silahaambazo Mungu ametupatia: Damu ya Mwana-Kondoo, naNeno la ushuhuda wetu. Tunapaswa kujifunza jinsi yakushuhudia kwa uaminifu kuhusu kila kitu ambacho damu yaYesu imefanya kwa ajili yetu.

Mwandishi Derek Prince aliweka muhtasari huu wa“Mwongozo wa Mafunzo ya Askari wa Mwisho wa Nyakati” ilikusaidia waamini kuelewa na kutumia nguvu ya damu yaYesu:

"Tunamshinda Shetani tunaposhuhudia binafsi kile ambachoNeno la Mungu linasema damu ya Yesu inafanya kwa ajili yetu." ( Ufunuo 12:11 )
"Kupitia damu ya Yesu, nimekombolewa kutoka mikononimwa Shetani." ( Waefeso 1:7 )
"Kupitia damu ya Yesu, dhambi zangu zote zimesamehewa." ( 1 Yohana 1:9 )
"Kupitia damu ya Yesu, ninaendelea kusafishwa kila sikukutoka dhambi zote."( 1 Yohana 1:7 )
"Kupitia damu ya Yesu, nimetangazwa kuwa mwenye haki —

nimesamehewa na kusimama mbele za Mungu kana kwamba

sikuwahi kutenda dhambi."( Warumi 5:9 )

"Kupitia damu ya Yesu, nimetakaswa, nimefanywa mtakatifu,na kutengwa kwa ajili ya Mungu."( Waebrania 13:12 )
"Kupitia damu ya Yesu, nina ujasiri wa kuingia katika uwepowa Mungu."( Waebrania 10:19 )
"Damu ya Yesu inanena kwa Mungu mbinguni kila mara kwaajili yangu." ( Waebrania 12:24 )

Sharti la Mwisho

Ufunuo 12:11 unahitimisha kwa sifa ya kipekeeinayowatofautisha wale wote wanaotoka wakiwa washindikatika pambano hili la kiroho:

“...wala hawakupenda maisha yao hata kufa.”

Tunawezaje kulihusisha jambo hili na maisha yetu?Inamaanisha kwamba kututii mapenzi ya Mungu ni jambo lamuhimu zaidi kuliko kubaki hai. Ikiwa tutajikuta katika haliambayo kuti totii Mungu kunamaanisha kupoteza maisha yetu, basi tutachagua kumtii Mungu bila kusita..

Labda sio sisi sote tutalazimika kufanya chaguo hili wazi.Lakini kinachohesabika mbele za Mungu ni kiwango chakujitoa kwetu. Uamuzi huo wa ndani unaleta nguvu ya kipekee katikaushuhuda wetu—nguvu ambayo Shetani hana silaha yakuipinga. Kwa hiyo, kila mmoja wetu anapaswa kujichunguzakwa uaminifu kwa kuuliza swali hili: “Je, ninaweza kusemakwa moyo wa kweli kwamba sipendi maisha yangu hatakufa?”?

4
Shiriki