Katika barua yangu iliyotangulia, nilieleza kwamba tunapokuwa Wakristo, tunajikuta moja kwa moja tukiingia katika vita vikubwa vya kiroho ambavyo vinavyoenea mbinguni na duniani. Zaidi ya hayo, adui zetu wenye nguvu na hatari zaidi ni ufalme wa malaika waovu ambao makao yao makuu yako katika ulimwengu wa mbingunii.

Kwa hekima na rehema zake Mungu ametupatia silaha zote tunazohitaji ili kupata ushindi. Kwa sababu vita vyetu viko katika ulimwengu wa kiroho, basi silaha zetu pia ni za kiroho. Katika 2 Wakorintho 10:4 Paulo anasema kwamba “silaha za vita vyetu si za mwili bali zina nguvu katika Mungu hata kuangusha ngome.”

Ngome tunazoshambulia pia ni za kiroho. Kwa karne nyingi Shetani amezijenga katika mioyo na akili za wanadamu. Ni ngome za hofu, tamaa, chuki, ibada ya sanamu, ubaguzi wa rangi, ushirikina wa kidini na mengine mengi.

Ni ngome hizi zinazokatisha juhudi zote za wanasiasa kujadili amani ya kweli. Hoja za kimantiki na za kisiasa zinazounga mkono mapatano yaliyojadiliwa hazina nguvu ya kutosha kuvunja ngome za kiroho zinazozuia amani.

Amani ya kweli itakuja duniani tu wakati ufalme wa Kristo utakaposimamishwa hapa. Hili ndilo lengo la vita vyetu kama Wakristo na kusudi la kutumia silaha zetu za kiroho. Ni kuvunja ngome za kiroho katika mioyo ya wanaume na wanawake na kuandaa njia kwa ajili ya Kristo kusimamisha ufalme Wake—kwanza katika mioyo yao na hatimaye katika dunia nzima.

Silaha Saba za Kiroho

Katika Waefeso 6:13–18 Paulo anaorodhesha silaha saba za kiroho—au vifaa vya kiroho—tunavyohitaji. Anatoa mifano yake kutoka kwa vifaa vya askari wa Kirumi katika siku zake. Ifuatayo ni orodha hio:

1. Mkanda wa ukweli (Mstari wa 14)

Katika siku za Paulo, wanaume na wanawake kwa kawaida walivaa mavazi marefu, yaliyolegea ambayo yalifika magotini mwao. Kabla ya kufanya kazi yoyote nzito au shughuli inayohitaji nguvu,jambo la kwanza walilopaswa kufanya lilikuwa ni kukusanya yale mavazi yao marefu na kuyatia ndani ya mkanda wao. Baada ya hapo ndipo waliweza kuwa huru kufanya kazi kwa bidii. Ndiyo maana tunasoma mara kadhaa katika Maandiko maneno haya: “Jifungeni viuno vyenu.”.

Kutumia mkanda wa ukweli kunamaanisha kuacha kila aina ya udanganyifu au maelewano na uovu. Tukishindwa 'kuyakusanya na kuyaweka kando' mambo hayo, yatatuzuia kusonga mbele kiroho. Tunapaswa kuwa waaminifu kwa ukweli wa Neno la Mungu hata pale unapokuwa wa utata au haukubaliki na watu wengi.

Kutumia mkanda wa ukweli kunamaanisha kuacha kila aina ya udanganyifu au maelewano na uovu. Tukishindwa kuyakusanya na kuyaweka kando mambo hayo, yatatuzuia kusonga mbele kiroho. Tunapaswa kuwa waaminifu kwa ukweli wa Neno la Mungu hata pale unapokuwa wa utata au haukubaliki na watu wengi.

“Basi wekeni mbali uovu wote, na hila zote, na unafiki, na husuda, na masingizio yote; kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa yasiyoghoshwa ya Neno, ili kwa hilo mpate kuokoka.”1

Zaidi ya yote, tunapaswa kuwa wazi kabisa na wa kweli katika mahusiano yetu na Mungu Mwenyewe. Hili ni sharti la kupokea ufunuo wa kiroho. Katika Zaburi 51:6 Daudi anasema:

“Angalia, wapendezwa na ukweli ulio moyoni, Na katika siri utanijulisha hekima.”

Mungu hudhihirisha hekima yake iliyofichika kwa wale tu walio na ukweli ndani ya mioyo yao.

2. Dirii ya Haki (mstari wa 14)

Hii hulinda moyo wetu. Katika Mithali 4:23 tunaonywa:

Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo, Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Mafanikio yetu katika maisha ya kiroho yanategemea kudumisha uhusiano mzuri wa moyo na Mungu pamoja na mwanadamu. Ni lazima tufuate kielelezo cha Paulo ambaye alisema kwamba anajitahidi “kuwa na dhamiri isiyo na lawama mbele za Mungu na mbele ya wanadamu sikuzote.”2

Aina ya haki Mungu anayoitazamia si tu kukubali mafundisho kwa akili. Ni hali ya moyo, si ya akili.

“Maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki...”3

Wala sio kufuata tu kanuni za kidini. Paulo mwenyewe alikuwa amejiweka katika ufuatiliaji wa sheria hizo kwa miaka mingi, lakini alipokutana na Kristo, nia yake ikabadilika:

“...ili nimwone Kristo na nionekane ndani Yake, nikiwa sina haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu kwa njia ya imani.”4

3. Viatu vya maandalizi ya injili ya amani (aya ya 15)

Askari wa Kirumi walivalishwa viatu imara sana ambazo ziliwapa uwezo mkubwa wa kusafiri haraka. Wangeweza kutembea eneo kubwa kwa haraka bila maandalizi ya muda mrefu.

Kama Wakristo, tunahitaji kuwa watu waliotayari kusonga— tukiwa tayari kwa ajili ya makusudi ya Mungu popote na wakati wowote anapotuita, hata bila taarifa ya mapema au katika hali zisizotarajiwa. Hii inahitaji maandalizi. Tunapaswa kufahamu ukweli wa msingi wa Injili na jinsi ya kuieleza kwa mtu asiyeamini.

Pia, ni injili ya amani. Tunaweza tu kuiwasilisha kwa ufanisi ikiwa tuna amani ya kweli mioyoni mwetu—amani isiyoyumba kutokana na hali za nje. Kwa mwenye dhambi aliye na wasiwasi na kuchanganyikiwa, sauti yetu yenye utulivu na upole inaweza kuwasilisha ujumbe wetu kwa ufanisi zaidi kuliko maneno tunayoyazungumza.

4. Ngao ya imani (Mstari wa 16)

Neno lililotafsiriwa hapa kama ngao linahusiana na neno mlango. Urefu wake ulikuwa mkubwa kuliko upana wake. Askari aliyefunzwa vizuri angeweza kuinama na kujikunja kiasi kwamba mwili wake wote ungebaki umefunikwa na kulindwa kabisa. Hata hivyo, alihitaji kuwa mwenye nguvu na mwili wenye wepesi; mtu aliyenenepa sana asingeweza kujikinga vizuri.

Vivyo hivyo, ngao yetu ya imani lazima iwe kamili katika vipimo vyake vyote. Inapaswa kufunika utu wetu wote—roho, nafsi, na mwili. Tunapaswa pia kuwa tumefunzwa kiroho kiasi kwamba tunaweza “kujikusanya” ndani ya eneo lililofunikwa kabisa na ahadi za Maandiko Matakatifu. Chochote katika maisha yetu ambacho ni cha kujipendekeza au kisichohitajika kitabaki nje ya ulinzi wa ngao hiyo.

Wakati mwingine mishale ambayo Shetani hutumia dhidi yetu ni “moto.” Mishale hii imewashwa moto, na madhumuni yake si tu kujeruhi bali pia kuwasha moto wa uharibifu mahali inapolenga. Inaweza kuchochea moto wa umbea, kashfa, au mgawanyiko ndani ya familia au hata kanisa zima. Lakini ngao ya imani — ikitumiwa kwa uangalifu na kwa ufanisi — si tu kwamba itazuia mishale hiyo, bali pia itazima kabisa moto wake..

5. Chapeo ya wokovu (Mstari wa 17)

Kama vile dirii inavyolinda moyo wetu, vivyo chapeo ya wokovu hulinda akili yetu—mawazo yetu. Akili ni eneo ambalo Wakristo wanashambuliwa mara kwa mara. Ndani ya akili zetu mara nyingi kuna vita vinavyoendelea. Shetani hutafuta kuingiza mawazo ambayo yatatuvuruga au kutukengeusha au kutufanya tushindwe kufanya kazi katika vita vyetu dhidi yake.

Mungu amenifundisha mimi binafsi masomo mengi katika eneo hili. Nilipookoka kwa mara ya kwanza, akili yangu ilikuwa inashambuliwa mara kwa mara na huzuni na kukata tamaa. Nilielewa kwamba nilihitaji ulinzi wa kudumu katika eneo hilo. Niliposoma orodha ya silaha za kiroho katika Waefeso 6:13–18, niligundua kwamba ilikuwa chapeo ya wokovu ambayo nilihitaji. Lakini nilijiuliza: “Najua kwamba nimeokoka. Je, hiyo inamaanisha tayari nina chapeo ya wokovu, au ni kitu ninachohitaji kupata baada ya wokovu?”

Nilipofikiria jambo hili, nikaona kuwa Wakristo wa Efeso ambao Paulo alikuwa akiwandikia tayari walikuwa wameokoka. Lakini bado Paulo aliwaagiza wachukue chapeo ya wokovu. Kwa hiyo, ni wazi kwamba nilihitaji kufanya vivyo hivyo. Lakini hii chapeo ya wokovu ilikuwa nini ambayo inapaswa kuwa ulinzi wa akili yangu?

Kwa bahati nzuri, nilikuwa nikitumia Biblia yenye marejeleo tofauti ukingoni. Rejeo kwa Waefeso 6:17 ilikuwa 1 Wathesalonike 5:8: “...na tumaini letu la wokovu kama chapeo.” Maandiko hayo yalibadilisha maisha yangu ya mawazo. Ikiwa kukata tamaa ilikuwa tatizo langu, basi matumaini ilikuwa suluhisho sahihi.

Nilianza kutafuta—na katika baadhi ya visa nikajifunza kwa moyo—mistari ya Maandiko iliyokuwa msingi wa matumaini imara na ya kudumu. Leo hii, akili yangu inalindwa kwa ufanisi!

Nilianza kutafuta—na katika baadhi ya visa nikajifunza kwa moyo—mistari ya Maandiko iliyokuwa msingi wa matumaini imara na ya kudumu. Leo hii, akili yangu inalindwa kwa ufanisi!kiroho na kushindwa kuendelea.

Sasa, tuangalie silaha mbili zilizobaki.

6. Upanga wa Roho (Mstari wa 17), ambalo niNeno la Mungu

Upanga huu unaweza kutumika kwa ulinzi na pia kwa mashambulizi, lakini kimsingi ni silaha ya kushambulia. Mtu mmoja aliwahi kusema: “Ulinzi bora zaidi ni kushambulia,” na mara nyingi hili ni kweli katika ulimwengu wa kiroho.

Neno lililotafsiriwa hapa kama “Neno” ni rhema, likimaanisha neno lililonenwa. Si Biblia iliyo kwenye rafu au mezani ndiyo yenye nguvu, bali ni pale tunapochukua Maandiko Matakatifu mdomoni mwetu na kuyatangaza kwa ujasiri kupitia midomo yetu—ndipo yanapogeuka kuwa upanga mkali wenye makali kuwili.

Zaidi ya hayo, Paulo anasema ni “Upanga wa Roho Mtakatifu.” Tunaweza kulitumia Neno la Mungu kwa maneno yetu, lakini linakuwa na nguvu kamili pale tu Roho Mtakatifu aliye ndani yetu ndiye anayelitumia.

Mfano kamili wa jinsi ya kutumia Upanga wa Roho unaonekana katika tukio la Yesu alipokutana na Shetani jangwani. Mara tatu Shetani alimjaribu Yesu, na kila mara Yesu alimshinda kwa maneno yale yale: “Imeandikwa.”5 Yesu hakutumia silaha nyingine ila rhema—neno lililonenwa la Mungu. Mungu ametupatia sisi Wakristo silaha hiyo hiyo.

Ni muhimu, hata hivyo, kukumbuka mambo mawili. Kwanza, Yesu alikuwa tayari “amejazwa na Roho Mtakatifu.”6 Ni Roho Mtakatifu ndani ya Yesu ambaye alimwongoza katika matumizi ya upanga.

Pili, Yesu alikuwa amehifadhi Maandiko moyoni Mwake. Kama kijana Myahudi wa wakati wake, alikuwa amekariri vifungu vingi vya Maandiko. Kwa hiyo, alipokabiliwa na Shetani, hakuhitaji kusoma vitabu au kutafuta rejeo—Neno lilikuwa tayari ndani Yake!

7. Maombi yote (Mstari wa 18)

Silaha hii ya saba haijaorodheshwa kwa namna ile ile kama zile sita za mwanzo, lakini ni muhimu sana kukamilisha vifaa vya askari wa Kikristo. Kati ya silaha sita za awali, Upanga wa Roho pekee ndio wa kushambulia na hata huo hufanya kazi kadiri mkono wa askari unavyoweza kufika.

Lakini silaha hii ya saba—maombi yote—haina mipaka. Tunaweza kuiita kama kombora la masafa marefu. Maombi yenye umakini, yanayoongozwa na Roho Mtakatifu, yanaweza kufika mabara mengine na kugonga shabaha kwa usahihi kamili. Bila shaka, hii ndiyo silaha yenye nguvu zaidi na yenye ufanisi mkubwa katika hazina ya silaha za Kikristo.

Kama ilivyo kwa Upanga wa Roho, maombi yote hupata ufanisi wake kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Lazima yaombewe “katika Roho.” Mungu hawezi kukabidhi silaha kama hii kwa Wakristo wanaoongozwa na tamaa au hisia za kimwili tu.

Maombi yote yanajumuisha aina nyingi tofauti za maombi—kama yale yaliyoorodheshwa katika 1 Timotheo 2:1: dua, maombi, maombezi na shukrani. Si sauti ya mtu mmoja pekee, bali ni waamini wengi wanaounganishwa kwa umoja na Roho Mtakatifu.

Wakati mwingine Mungu huruhusu vikwazo vikubwa vinavyoonekana haviwezekani ili kuamsha maombi ya aina hii. Katika Matendo 4:15–18, mitume walikabiliwa na hila ya kishetani iliyoweza kusitisha kabisa kazi ya Injili. Baraza la Wayahudi, mamlaka ya juu ya kidini, liliamuru rasmi kwamba, mitume “wasiseme kabisa wala wasifundishe katika jina la Yesu.”

Wapinzani wa Injili walitambua umuhimu wa kipekee wa Jina la Yesu, kwa kuwa:

“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”8

Kwa amri hii ya baraza, Shetani alikuwa amejenga “ngome” ambayo ingezuia maendeleo zaidi ya injili au ukuaji wa kanisa changa.

Lakini waamini wote walikusanyika pamoja kuomba msaada wa Mungu. Wakiwa kama orkesta moja, walimlilia Bwana kwa nguvu. Mungu alijibu kwa onyesho la nguvu zake, kwani: “Mahali walipokuwa wamekusanyika pamoja pakatikisika; wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakalinena Neno la Mungu kwa ujasiri.”9 Silaha ya maombi yote ilikuwa imebomoa ngome ya Shetani.

Leo hii, katika sehemu nyingi duniani, Shetani ameunda vikwazo na upinzani vinavyozuia maendeleo ya Injili. Njia za kawaida za uinjilisti haziwezi kuvivunja. Ni wakati sasa wa kanisa kutumia silaha yake yenye nguvu zaidi — silaha ya maombi yote.

Mada ya barua yangu inayofuata—na ya mwisho—katika mfululizo huu itakuwa Kilele cha Mapambano.

12
Shiriki