Katika kutoa maagizo kuhusu mwenendo wa ibada katikakanisa la Agano Jipya, Paulo anaandika: “Kwa sababu hiyoimempasa mwanamke kuwa na alama ya mamlaka juu yakichwa chake, kwa ajili ya malaika.”

Wakristo wanapokutanakwa ajili ya ibada, malaika pia watakuwepo na watashiriki.

Zaidi ya mara moja mimi na Ruth tulipokuwa tukiabudupamoja, alisikia malaika wakiimba. Tulitambua kwambatulikuwa na pendeleo la kujionea sehemu ndogo ya ibadakamili ya ulimwengu wote mzima, inayoanzia mbingu nadunia pia. Nimesikia ushuhuda kama huo kutoka kwaWakristo wengine.

Katika Waebrania 1:14 mwandishi anasema kwamba malaikawa Mungu ni “roho watumikao waliotumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu.” Maneno ya Kigirikiyanayotafsiriwa “roho watumikao” hufafanua hasa rohozinazofanya matendo ya ibada ya kikuhani. Katika Kanisa laAgano Jipya mbingu na nchi ziliunganishwa pamoja katikaibada.

Maasi ya Malaika Yanayofuatana

Biblia inafunua mfululizo wa uasi wa kimalaika dhidi yaMungu. Uasi wa kwanza—na wa maana zaidi—ilikuwa ni uasiwa awali wa Lusifa (malaika mkuu) unaoelezwa katika Isaya14:12–14:

“Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,

ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko!Umetupwa chini duniani,wewe uliyepata kuangusha mataifa!Ulisema moyoni mwako,“Nitapanda juu hadi mbinguni,nitakiinua kiti changu cha utawala juu ya nyota za Mungu;nitaketi nimetawazwa juu ya mlima wa kusanyiko,kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu.Nitapaa juu kupita mawingu,

nitakuwa kama [sawa na] Aliye Juu.’”

Kwa upande wangu, ninaamini kwamba Mtu wa Kiunguambaye Shetani alitamani cheo chake hakuwa Mungu Bababali Mungu Mwana (aliyefunuliwa baadaye katika historia yabinadamu kama Yesu wa Nazareti). Mgogoro kati ya hawawawili ulifikia kilele chake msalabani, ambapo shetanialionekana kana kwamba amemshinda Yesu, lakini kwa kweliYesu alimvua shetani silaha zake zote na kumwacha akiwaameshindwa kabisa. “Akiisha kuzivua enzi na mamlaka [zashetani], alizifanya kuwa dhihaka hadharani, akizishinda kwanjia ya msalaba.”2

Katika Ufunuo 12:3–4 Shetani anaonyeshwa kama “jokakubwa jekundu” ambaye “mkia wake ulikokota theluthi mojaya nyota za mbinguni.” Yaonekana kama malaika mkuu,Lusifa (sasa Shetani) alikuwa na mamlaka juu ya theluthi mojaya malaika wa mbinguni, ambao walimfuata katika uasi wakena walikuwa pamoja naye kutupwa kutoka mbinguni. Shetanina malaika waliomfuata kisha wakasimamisha ufalmeunaoshindana katika “mahali pa mbinguni,”3 mahali fulani katiya mbingu ya tatu4 (palipo makao ya Mungu) na mbinguinayoonekana kutoka duniani.

Ingawa hatima ya shetani imekwisha amuliwa kabisa kupitiakushindwa kwake msalabani, hukumu ya mwisho juu yakehaitatekelezwa hadi mwisho wa utawala wa miaka elfu moja.Wakati huo, shetani—pamoja na mpinga Kristo—wata “tupwakatika ziwa la moto na kiberiti... nao watateswa mchana nausiku milele na milele.”5

Malaika Walioanguka Kabla ya Gharika

Uasi mwingine wa malaika unaelezwa katika Mwanzo 6:1–2:

“Idadi ya watu ilipoanza kuongezeka duniani, na watoto

wa kike wakazaliwa kwao, wana wa Mungu wakawaonakuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura,

wakaoa yeyote miongoni mwao waliyemchagua.”

Hawa “wana wa Mungu” ni nani? Wametajwa mara mbilikatika kitabu cha Ayubu.

Katika Ayubu 1:6: “Siku moja wana wa Mungu waliendakujionesha mbele za Bwana. Shetani naye akaja pamoja nao.”

Na tena katika Ayubu 38:7 Mungu anapomuuliza Ayubu:“wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na malaika wotewalipokuwa wakishangilia kwa furaha?”

Kwa hakika, katika vifungu hivi vyote viwili “wana wa Mungu”walikuwa viumbe wa kimalaika. Hakika hakuna mwanadamualiyekuwepo wakati Mungu alipoweka msingi wa dunia.

Kuna vifungu viwili katika Agano Jipya vinavyoelezea hukumuya Mungu juu ya malaika waliofanya dhambi kwa njia hii nawanawake wanadamu. Katika Yuda 6 inasema: “Nao malaikaambao hawakulinda nafasi zao, lakini wakayaacha makaoyao, hawa amewaweka katika giza, wakiwa wamefungwakwa minyororo ya milele kwa ajili ya hukumu Siku ile kuu.”

Ni wazi kwamba hawa si malaika waliokuwa sehemu ya uasiwa awali wa shetani, kwa maana shetani na malaika zakebado hawajafungwa, bali wako huru na wanaendelea kutendakazi “katika ulimwengu wa roho.” Dhambi ya malaika ambaoYuda anawaelezea ni kwamba waliacha makao yaowaliyopewa mbinguni na kushuka duniani, ambako waliishi nawanawake wa kibinadamu..

Yuda aendelea kusema: “Vivyo hivyo, Sodoma na Gomora napia ile miji iliyokuwa kandokando, ambayo kwa jinsi moja nahao, walijifurahisha kwa uasherati na kufuata tamaa za mwilizisizo za asili, waliwekwa wawe mfano kwa kuadhibiwakatika moto wa milele.”

Yuda anawalinganisha malaika walioanguka wakati wa Nuhuna watu wa Sodoma na Gomora kwa sababu makundi yotemawili yalihukumiwa kwa dhambi ile ile ya uasherati naupotovu wa maadili.

Katika 2 Petro 2:4–6, mtume pia anaunganisha pamojamalaika walioanguka wakati wa Nuhu na watu wa Sodoma naGomora:

“Kwa maana, kama Mungu hakuwasamehe malaika

walipotenda dhambi, bali aliwatupa Kuzimu katikavifungo vya giza wakae humo hadi ije hukumu; kamahakuusamehe ulimwengu wa kale alipoleta gharika juuya watu wale wasiomcha Mungu, lakini akamhifadhiNuhu, mhubiri wa haki, pamoja na watu wengine saba;kama aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kwakuiteketeza kwa moto ikawa majivu, na kuifanya kuwakielelezo kwa yale yatakayowapata wale wasiomcha

Mungu...”

Katika hali zote mbili dhambi yao ilikuwa ngono isiyo yakawaida. Katika mstari wa 4, ambapo tafsiri inasema,“watupeni kuzimu,” neno la Kigiriki lililotumiwa ni tartarus,neno linalopatikana mara nyingi katika fasihi ya Kigiriki.Tartarus limefafanuliwa kuwa “mahali pa kifungo kilicho chinizaidi ya Kuzimu, kama vile Kuzimu ilivyo chini ya dunia.”

Ni jambo la kushangaza kuona ni kwa muda gani Bwanahuvumilia baadhi ya aina za dhambi ulimwenguni, lakini kunamipaka fulani ambayo Mungu huilinda kwa wivu mkubwa.Moja ya mipaka hiyo ni ile inayokataza upotovu wakingono—iwe ni kati ya malaika na wanadamu, au kati yawanadamu wa jinsia moja. Wakati mpaka huo unapovunjwa,hukumu kali zaidi za Mungu hufuata haraka. Katika tukiomoja, hukumu ilikuja kwa njia ya gharika, na katika jingine,hukumu ilifuta mara moja wakaaji wote wa miji miwili kwapamoja waliangamia.

Dhambi Zinazofanana Katika Siku Zetu

Biblia inaonyesha wazi kwamba mahusiano ya kingono katiya malaika na wanawake wa kibinadamu hayakuisha kabisawakati wa gharika. “Majitu yalikuwepo duniani siku zile—nahata baada ya hapo—wakati wana wa Mungu walipoingiakwa binti za wanadamu, wakazaa nao watoto. Hao walikuwamashujaa wa zamani, watu maarufu.”6

Neno la Kiebrania majitu (nephilim) limetokana moja kwamoja na kitenzi cha Kiebrania naphal, ambalo maana yake ni“kuanguka.” Hivyo basi, majitu ni “waliyoanguka,” yaani,malaika waliyoanguka. Kulikuwa na majitu duniani “siku zile”(yaani, wakati wa gharika) — na hata baada ya hapo (yaani,baada ya gharika).

Wale waliozaliwa katika kipindi hiki cha baadaye kupitiamuungano huu usio wa kawaida waliitwa mashujaa. Hadithiza Kigiriki zimejaa maelezo kuhusu mashujaa kama hao.Walisemekana kuwa walizaliwa wakati viumbewaliotambuliwa na Wagiriki kama “miungu” walipokuwa namahusiano ya kingono na wanawake wa kibinadamu. Miunguhii ilikuwa ni viumbe wenye nguvu za kimiujiza walioteremkakutoka katika kiwango cha juu cha uhai. Biblia inawaita majitu— ambao, kwa hakika, walikuwa malaika walioanguka.

Kwa kutoa mifano michache tu: Zeus (anayejulikana kama“baba wa miungu”) alisemekana kujigeuza kuwa bata mzingana kuungana na mwanamke aitwaye Leda, ambaye alizaanaye watoto watatu. Wakati mwingine, akiwa katika umbo lang’ombe dume, Zeus akawa na mahusiano na Europa, nayepia akamzalia wana watatu. “mungu” mwingine—Poseidon,mungu wa bahari—aliungana na mwanamke wa kibinadamuna wakazaa mtoto aitwaye Theseus, ambaye alikujakujulikana kama mmoja wa mashujaa mashuhuri wa Ugiriki.

Mifano mingine mingi inaweza kutolewa. Hadithi hizi ni kamakioo kilichopasuka, kinachoonyesha picha iliyopotoka yamatukio ambayo yameelezwa kwa usahihi katika Mwanzo6:4.

Kama katika Siku za Nuhu

Katika Luka 17:26 Yesu anatuonya: “Kama ilivyokuwa siku zaNuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana waAdamu.” Kwa maneno mengine, hali zilizokuwapo katika sikuza Nuhu zitajitokeza tena katika kipindi cha kabla ya enzi yasasa kufika mwisho.

Katika siku za Nuhu, “dunia ilikuwa imeharibika mbele zaMungu, nayo dunia ikajaa udhalimu.”7 Hakika, mambo hayamawili yanaonekana waziwazi tena mbele ya macho yetuleo—upotovu wa maadili na kuongezeka kwa vurugu naghasia bila kikomo.

Katika siku za Nuhu pia, wanadamu walivamiwa na malaikakutoka ngazi ya juu zaidi waliowafanya wanawake wakibinadamu kuwa chombo cha tamaa zao. Leo hii tena,vyombo vya habari vimejaa ripoti kuhusu “wageni kutokaanga za juu.” Wakati mwingine, matukio haya yanathibitishwana mashahidi waliotoa maelezo ya moja kwa moja yawalichokiona.

Tunaweza kuyatupilia mbali maelezo haya tukiyaita hadithi zakubuniwa, lakini hilo halielezi kwa nini matukio kama hayayanaendelea kuongezeka kwa kasi. Ufafanuzi mwingineunaopendekezwa na Maandiko ni kwamba hali za siku zaNuhu zinajirudia. Malaika walioanguka wako tena kaziniduniani.

== Neno la Wakati Mwafaka kutoka kwaPaulo ==

Ikiwa tafsiri iliyo hapo juu ya Maandiko ni sahihi, basi inatupamsisitizo mpya kwa onyo la Paulo lililotolewa katika 1Wakorintho 11:2–16. Paulo hakuliona Kanisa kama kundi dogola watu waliotengwa katika jengo fulani la kidini. Bali alionaKanisa kama sehemu ya tamasha kubwa lenye matukio mengiyanayoenea duniani na mbinguni. Ushiriki katika mikutanoyao haukuhusu wanadamu pekee, bali pia uliwezakujumuisha malaika, wema na waovu.

Hasa, Paulo alionya kwamba wanawake wanaoshiriki katikaibada ya kanisa walipaswa kutambua uwezekano wa uwepowa malaika wema na waovu. Jibu lao sahihi lilikuwa kufunikavichwa vyao. Kwa kufanya hivyo, walithibitisha kwamba wakochini ya mamlaka ambayo Kristo ameikabidhi Kanisa Lake. Piawaliwapa heshima inayostahili malaika wema waliokuwepo,na wakati huohuo walijilinda dhidi ya ushawishi wa kiroho usio safi unaoweza kutoka kwa malaika waovu.

Maagizo kuhusu ibada ambayo Paulo anatoa katika 1Wakorintho 11:2–16 yanaweza kufupishwa kwa neno moja:heshima.

“Heshima Yangu Iko Wapi?”

Wakati wa nabii Malaki, Bwana aliwashutumu watu Wake kwakukosa uaminifu katika ibada yao. Walikuwa watu wa dinisana, lakini walikosa heshima. Katika Malaki 1:6, Bwanaasema:

“Mwana humheshimu baba yake,

naye mtumishi humheshimu bwana wake.

Kama mimi ni baba, iko wapi heshima ninayostahili?

Na Kama mimi ni bwana,iko wapi heshima ninayostahili?”Kisha katika Malaki 1:14 anamalizia:

“Kwa kuwa mimi ni Mfalme Mkuu, nalo Jina langulinapaswa kuogopwa miongoni mwa mataifa.”

Katika karibu tamaduni zote, kuna kanuni fulani za mwenendozinazodhibiti jinsi watu wanavyohusiana na mfalme wao.Kanuni hizi huitwa itifaki.

Kama ilivyo kwa mfalme wa kidunia, Bwana naye ana itifakiYake. Baadhi ya masharti ya itifaki ya mbinguni yameelezwakatika 1 Wakorintho 11:2–16. Masharti haya yanatukumbushakwamba Wakristo wanapomwabudu Mungu, si kundi dogolililojitenga peke yao. Kinyume chake, Paulo anasema,

  • “Tumekuwa kama tamasha kwa ulimwengu [ulimwengu

mzima], kwa malaika na kwa wanadamu.”*8 Tumeonakwamba neno “malaika” linajumuisha malaika wema nawaovu.

Kama ishara ya heshima yetu kwa Bwana, na pia kwamanufaa yetu wenyewe, tunapaswa kujifunza na kufuatamasharti ya itifaki ya mbinguni..

Mada ya barua yangu inayofuata itakuwa Vita Katika Maeneoya Mbinguni.

16
Shiriki